MICHEZO
Gwiji wa Soka nchini Ufaransa Marcel Desailly ameiambia Sport1 kuwa Zidane anapswa kuwa makini endapo mpango wa kupewa nafasi ya kuwa kocha mkuu FC Bayern Munich utafanikiwa kama inavyotajwa katika vyombo kadhaa vya habari nchini Ujerumani.
Amesema Kocha huyo ambaye alicheza naye kwenye kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Ubingwa wa Dunia mwaka 1998, anapaswa kuwa makini katika usajili wa wachezaji na kuwaondoa baadhi ambao kwa sasa hawana msaada kwenye klabu ya FC Bayern Munich.
“FC Bayern Munich ina wachezaji wachache wanaozoea falsafa ya Zidane na 4-3-3 yake. Klabu inapaswa kutumia pesa nyingi kurekebisha timu na kuibadilisha kulingana na mahitaji yake.
“Lakini kwa nini usifanye hivyo? Ikiwa Bayern kweli wanataka mabadiliko makubwa hii itakuwa fursa sahihi. Lakini hii itategemea na usajili atakaoufanya na kuwaacha baadhi ya wachezajia mbao wanaonekana hawana msaada.”