MICHEZO
Licha ya kufungwa mabao 5-0 na Arsenal juzi Jumanne (Aprili 23), Uongozi wa Klabu ya Chelsea bado haijaamua mustakabali wa Kocha Mkuu wa kikosi chao Mauricio Pochettino.
Gazeti la Telegraph la nchini England limeandika kuwa Kocha huyo kutoka nchini Argentina, bado anaungwa mkono na Uongozi wa klabu hiyo, na huenda akawa ushirikiano mkubwa kuelekea msimu ujao 2024/25.
Gazeti hilo limeandika:
“Chelsea inakabiliwa na fumbo kubwa au uamuzi mbaya juu ya mustakabali wa Kocha Mkuu Mauricio Pochettino huku wachezaji wa klabu hiyo wakijiandaa kwa msimu mwingine wa msukosuko.
“Telegraph Sport inaelewa kwamba hakuna uamuzi wa wengi ambao umechukuliwa kuhusu ikiwa Pochettino atasalia kazini au la hadi mwisho wa msimu huu, licha ya kushindwa kutoboa katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la FA kwa kuchapwa Manchester City na kisha Arsenal Jumanne (Aprili 23) usiku.
“Presha inaongezeka kwa Pochettino huku kukiwa na kuchanganyikiwa kwa baadhi ya maamuzi, lakini bado anaendelea kuungwa mkono ndani ya Chelsea na inatambulika kwamba amekuwa akifanya kazi katika mazingira magumu.
“Pia kuna imani kwamba Pochettino hawezi kuwajibika tu kwa matatizo ambayo Chelsea inakabili kwa sababu hakuwajibika kwa sera ya uhamisho na uamuzi wa kuunda kikosi cha vijana kama hicho.”