WACHEZAJI CHELSEA SABABU YA POCHETTINO KUWA SALAMA

0:00

MICHEZO

Wachezaji wa Chelsea bado wanamuunga mkono Kocha wao mkuu, Mauricio Pochettino licha ya matatizo yao msimu huu, kwa mujibu wa ripoti.

‘The Blues’ wanaweza kumaliza msimu wakiwa nje ya katika nafasi ya kufuzu Ligi ya Europa mwaka wa pili mfululizo, baada ya kudhalilishwa kwa mabao 5-0 na wapinzani wao Arsenal, huku Jumamosi wakitoka sare ya 2-2 na Aston Villa.

Shinikizo linaongezeka kwa Pochettino, kocha huyo mwenye umri wa miaka 52, bado anaheshimiwa sana katika chumba cha kubadilishia nguo, huku Standard ikiripoti kuwa wachezaji wanamuunga mkono.

Nahodha Reece James na msaidizi wake, Ben Chilwell, wameshindwa kutoa ushawishi na usaidizi mkubwa kwa kocha Pochettino kama walivyotarajia, kutokana na majeraha.

Baadhi ya wajumbe wa bodi wanaamini Pochettino anastahili kuendelea na nafasi yake kuelekea msimu ujao, kwani wanatambua changamoto alizokabiliana nazo na kupongeza juhudi zake za kuvuka mazingira magumu.

Muargentina huyo alisaini mkataba wa miaka miwili na Chelsea msimu uliopita wa majira ya joto ambao ulijumuisha chaguo la miezi 12 zaidi.

Na kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu huu, Pochettino atakuwa akitumia kila juhudi kudumisha nafasi yake katika kiti cha moto huko London Magharibi.

Anabakia na imani kwamba mbinu zake hatimaye zitaleta majibu kama ilivyokuwa wakati akiwa na kikosi cha vijana cha Tottenham Hotspur.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

leo
tu
Read more
MFAHAMU OSMAN BEY KIPENZI CHA WAPENDA FILAMU...
NYOTA WETU Burack Ozcivit wengi mnamfahamu kama Osman Bey kama...
Read more
WASANII WA KIKE TANZANIA WALIOFANYA VIZURI 2023...
MICHEZO Orodha ya wasanii 5 hapa Tanzania wanaofanya vizuri kwenye...
Read more
DAVIDO LAUNCHES NEW COURSE AT UNIVERSITY OF...
OUR STAR 🌟
See also  SABABU YA KIFO CHA PETER "Peetah" MORGAN HII HAPA
Nigerian singer and songwriter David Adedeji Adeleke,...
Read more
Kenya Power Announces Planned Power Interruptions Across...
Kenya Power has announced upcoming power cuts scheduled to take...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply