MICHEZO
Kocha wa Klabu ya Manchester United, Erik Ten Hag amekiri kuwa mchezaji wake, Jadon Sancho ambaye kwa sasa anakipiga kwa mkopo kunako klabu ya Borusia Dortmund ya Ujerumani, jana alionesha kiwango kizuri kwenye mchezo wa nusu fainali ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya PSG.
“Acha niseme hili, jana Sancho amecheza vizuri sana. Ni mchezaji mzuri sana. Jana ameonesha kwa nini Manchester United walimnunua na alionesha anaiwakilisha thamani kubwa ya Manchester United, kitu ambacho ni bora zaidi.
“Nimefurahishwa na Sancho kwa kiwango cha jana, tutaona kitu gani ambacho kitatokea mbeleni,” amesema Ten Hag.
Sancho alirejea kwenye timu yake ya zamani ya Dortmund kwa mkopo Januari 11, 2024 baada ya kuondolewa na kocha Ten Hag kwenye kikosi cha Man United kwa makosa ya kinidhamu.
Sancho amekuwa na mwendelezo mzuri wa kiwango katika timu ya Dortmund katika mechi za hivi karibuni.