MICHEZO
Nyota wa Yanga SC, Joseph Guede ambaye alisajiliwa katika dirisha dogo ameitumikia timu hiyo kwa dakika 743, kwenye NBC Premier League na kucheka na nyavu mara nne.
Mbali na kwenye NBC PL, mchezaji huyo raia wa Ivory Coast pia ameshacheka na nyavu mara tatu kwenye michuano ya CRDB Bank Federation Cup ukiwemo mchezo wa jana wa robo fainali dhidi ya Tabora United.
Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Guede pia ameacha alama kwa kufunga goli moja kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya CR Belouizdad uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.
Kwa mwenendo wa mchezaji huyu tangu ametua, ameanza kukonga nyoyo za wapenda soka nchini Tanzania na kwa wafuatiliaji wa soka na vilabu vya Tanzania walioko nje.