NYOTA WETU
“WEWE NDIO DUNIA YANGU CHOCHOTE WACHUKUE WANIACHIE WEWE “BABA KEAGAN”
Ujumbe mzito wa Baba KEAGAN Paul Makonda kwenda Kwa Mkewe akimtakia Kheri ya Siku yake ya Kuzaliwa
“Dunia imebeba Mengi sana ila mimi nimekubali kubebwa nawe kipenzi changu, kwani wewe ndiye Dunia yangu, chochote wachukue lakini waniachie wewe, Maria wangu, mwanamke wa maisha yangu, NAKUPENDA MNOO!! ninaamini MUNGU hutubariki, lakini Baraka zake hupitia kwa watu, wewe ndio yule mtu, uliebeba za kwangu, ambae kupitia wewe naona vingi maishani mwangu, nataka nikwambie jambo moja, unapendwa mnoo na Makonda, popote unapopita ringa na tembea kifua mbele ukiamini Hakuna mwanaume anaekupenda kama mimi, kwako hata ashushwe mwanamke wa namna gani na asemwe kwa sifa zote za uzuri bado nakiri hakufikii, kwako sioni sisikii, Nakupenda mnoo, na katika siku yako hii kubwa nataka nikwambie MOYO wangu unao wewe, Happy Birthday kipenzi changu, Mama wa watoto wangu, nakuombea umri mrefu ili niendelee kufaidi Nuru ya uzuri wako kwenye himaya yangu, hapa ni KUFA “.