SABABU JOSEPH SELASINI KUMLIPA JAMES MBATIA MILIONI 80

0:00

HABARI KUU

Aliyekuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ameshinda kesi dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Joseph Selasini ambaye alimfungulia mashtaka ya udhalilishaji dhidi yake.

Hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemwamuru Selasini kumlipa Mbatia kiasi cha shilingi milioni 80 kama fidia ya kumchafua, kulipa gharama za shauri pamoja na kumwomba radhi.

Wakili wa Mbatia, Hudson Mchau amesema hukumu hiyo imetolewa Mei 02, 2024 chini ya Hakimu Aron Lyamuya kufuatia maneno ya kashfa na udhalilishaji aliyoyasema Selasini dhidi ya Mbatia akiwa katika mkutano mjini Musoma mkoani Mara.

”Mahakama iliamuru kwamba maneno alioyaongea ndugu Joseph Selasini huko Musoma yalikuwa ni maneno ya udhalilishaji hivyo iliamuru aweze kuomba radhi ‘either’ [ama] kwa kwenda Musoma alipoweza kutoa maneno yale au aweze kutoa katika gazeti ambalo linasambazwa na eneo kubwa la nchi katika ukurasa wa mbele,” amesema.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Gideon Kimaiyo yuko tayari Kuoa
Mbunge wa Keiyo Kusini, nchini Kenya, Gideon Kimaiyo, aliapa kwamba...
Read more
TV presenter Laura Woods has revealed she...
They each won gold in their respective weight divisions at...
Read more
Austria back in business, says Arnautovic after...
Austria captain Marko Arnautovic said his side are playing like...
Read more
WAYS ON HOW TO SHOW TRUE LOVE...
LOVE TIPS ❤ 12 WAYS ON HOW TO SHOW YOUR...
Read more
portland Will be the third Expansion...
Portland, Oregon, has become the latest city to benefit from...
Read more
See also  UGANDA YAZINDUA MFUMO WA KUZUIA RUSHWA

Leave a Reply