TUNDU LISSU AMSHTUKIA MBOWE KUELEKEA 2025

0

0:00

HABARI KUU

Baada ya Lissu kutangaza jukwaani kuwa rushwa imekithiri kwenye uchaguzi wa ndani wa CHADEMA, hali hiyo imevuta hisia za wengi na kuleta taswira ya vita ya madaraka kati yake na Freeman Mbowe wakati huu ambapo maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa  na uchaguzi mkuu wa mwakani yakiendelea.

Madai ya Lissu aliyatoa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Mkoani Iringa, na kuibua sintofahamu ya mgogoro huo wa maslahi huku wengine wakihisi huenda ni vita ya ni nani ateuliwe na CHADEMA kuwania urais mwaka 2025 kati ya Lissu na Mbowe.
Ā 
Alisema, “kuna mtafaruku mkubwa sana wa uchaguzi ndani ya chama chetu, kuna pesa nyingi ajabu kwenye uchaguzi huu (ndani ya CHADEMA),” madai ambayo yanaenda sambamba naĀ Lissu kulalamika kuwa amekuwa akiambiwa na uongozi wa chama chake kuwa hakuna pesa za kulipia mikutano yake ya hadhara, lakini anashangaa kuona kuna pesa za rushwa kwenye uchaguzi wa ndani.

Kitendo cha Lissu kulalamika hadharani kuhusu rushwa ndani ya chama na kunyimwa pesa za maandamano na mikutano ya hadhara, kimetafsiriwa na baadhi ya Wanachadema kama ni utovu wa nidhamu na kukidhalilisha chama.

Wamedai kuwa utaratibu wa CHADEMA ni kuwa kiongozi huyo alitakiwa kuwasilisha malalamiko yake kwenye vikao rasmi vya ndani vya chama, ikiwemo Kamati Kuu, siyo jukwaani.

Mbowe na Lissu kwa nyakati tofauti wote  wamewahi kugombea urais mara moja na kushindwa na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na taarifa kutoka ndani ya CHADEMA zinasema Mbowe na Lissu wote wanataka kugombea urais kupitia chama hicho mwaka 2025 na hiyo ndiyo sababu kuu ya mtafaruku ndani ya chama hicho.

See also  Mwili wa Ebrahim Raisi wapatikana

Aidha, inadaiwa kuwa pia licha ya uongozi wa CHADEMA kumkataza Lissu asifanye mkutano Iringa, asubiri hadi uchaguzi wa ndani upite, Lissu alikaidi maagizo ya chama huku akiwataka wanaCHADEMA nchi nzima kutochagua viongozi wanaotumia pesa kwenye uchaguzi.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini wanasema kuwa vita ya Mbowe na Lissu inatarajiwa kupamba moto zaidi siku zijazo, kwani mafahali hao wawili hawawezi kuishi kwenye zizi moja.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading