0:00
MICHEZO
Washika mitutu wa London, Arsenal wameendeleza matumaini yao ya kutwaa taji la ligi kuu ya kandanda nchini England baada ya kuiangushia kipondo AFC Bournemouth kwa kuwakanda 3-0 katika mchezo wa muendelezo wa ligi hiyo
Ushindi huo umeifanya Arsenal kufikisha alama 83 kileleni kwenye msimamo baada ya michezo 36, huku wakiendeleza dua mbaya kwa Manchester City walio katika nafasi ya pili na alama 79 baada ya michezo 34.
Arsenal imebakiza michezo miwili kutamatisha ligi hiyo ambapo watasafiri kuwafuata Manchester United Old Trafford na kisha kumalizia nyumbani dhidi ya Everton
Wakati Man City wao wakisaliwa na michezo minne.
Related Posts 📫
Leicester City coach Steve Cooper says he is happy to...
SEVILLE, Spain, 🇪🇸 - Atletico Madrid's unbeaten run in LaLiga...
Mikel Arteta will hope to add to his squad to...