MAKALA
Pichani ni Carlos Sylvester [Mastermind], Agent wa wachezaji mbalimbali kwenye ligi yetu akiwa na viongozi wa Timu za Simba na Yanga.
Pale Yanga anawasimamia wachezaji wawili, Bakari Nondo Mwamnyeto na Gift Mauya na Simba ana wachezaji wanne ambao ni Mzamiru Yassin,Kibu Denis, Mohamed Hussein na Hussein Kazi.
Kibu Denis,Mzamiru Yassin na Mwamnyeto mikataba yao inaelekea mwishoni, Carlos anafahamu huu ndio wakati wa kutengeneza pesa kupitia wateja wake.
Katika nyakati hizi ni rahisi sana kusikia Mwamnyeto anataka kwenda Simba na Kibu Denis anataka kwenda Yanga ilimradi tu ‘Mteja’ apate thamani anayoitaka Agent.
Iko hivi…
Kwenye kujadili mkataba mpya wa Kibu Denis ni rahisi sana Simba kuulizia uwezekano wa kumpata NONDO na pia Yanga wanapojadili namna ya kuongeza mkataba wa Mauya ni rahisi kuulizia huduma ya Kibu,Zimbwe au Mzamiru.
Hapa ndipo tetesi zinapozaliwa na kusambaa…
Mfano, Simba wako tayari kumpa Kibu Denis mkataba mpya wenye thamani ya Tsh 300m kutoka 200m sambamba na nyumba na bonus zenye thamani ya Milioni 600 kwa miaka miwili…
Unadhani kwanini Kibu hajasaini…?
Carlos anasubiri upepo sehemu nyingine, kashikilia Ofa ya Simba halafu anaulizia sehemu nyingine kama wanaweza kuongeza Dau kulifikia au kuzidi.
Kama Yanga watasema wako tayari kumpa 350, maana yake Carlos atarudi kwa Simba kuwambia kuwa Yanga kaweka 350m nyie Mnasemaje?
Simba akiona bado anamhitaji Kibu ataongeza 20-50m itafika 400m, Carlos atarudi tena Yanga!
Yaani kipindi hiki ni kama madalali wanavyouza nyumba za Benki tu…
Tetesi hazikwepeki na sio kila tetesi isipokua kweli ionekane alieileta ni wa MCHONGO…
Ni mfumo tu wa biashara ya Mpira ilivyo.