CHARLES KITWANGA awatetea polisi kuhusu rushwa na kuwabambikia raia kesi

0:00

NYOTA WETU

Mwanasiasa wa siku nyingi na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini, Charles Kitwanga amekemea tabia ya kuwalaumu Polisi moja kwa moja kuhusu mapungufu ya huduma yaliyopo katika utendaji wao wa kazi ikiwemo uadilifu, huku akitaka jamii inayohudumiwa na wanausalama hao kujitambua, ili kuleta mabadiliko.

Kitwanga aliyasema hayo katika mahojiano maalumu aliyowahi kuyafanya nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na kusema lawama nyingi zimekuwa zikitolewa kwa Jeshi hilo, kutokana na baadhi ya matendo yasiyokuwa na uadilifu ambayo hayana ulazima na kwamba, ili kubadili dhana hiyo jamii haina budi kuanza yenyewe kubadilika.

Amesema, “nani wanaotoa lawama, si ni Watanzania ambao Polisi wanawahudumia. Kuna pande mbili Polisi na raia, niwe mkweli ukiwalaumu Polisi moja kwa moja unakosea kwanini sisi tunaohudumiwa tusijitambue na jambo moja ambalo linapenda kutajwa sana ni rushwa na katika hilo kuna mpokeaji na mtoaji, hivi mtoaji akikataa kuroa rushwa mpokeaji atapataje?.”

Kuhusu kubambikia kesi raia, Kitwanga amesema ukiliangalia suala hilo kwa undani halianzi kienyeji bali kuna sababu ambazo huenda zinaanzia katika ugomvi wa mtu na mtu na kisha kutumia Polisi kwa kufahamiana, ili kumpa kesi ya uongo mshitakiwa, hivyo amewataka Watanzania kubadilika na kumtanguliza MUNGU mbele.

“Hawa Askari ni Wafanyakazi, sikatai anaweza kuwepo ambaye nidhamu yake si nzuri sana akafanya tendo kama hilo ukichukua makosa ya watu walio gerezani unaweza kuona ni wangapi wamebambikiziwa na wangapi wana makosa ya kwao, nilishangaa majuzi mtu ametoka kwa msamaha wa Rais baada ya wiki moja amerudi tena ndani sasa huyo amebambikiziwa? ni lazima Polisi wetu wawe na nidhamu lakini na sisi Watanzania tuwe wakweli,” alisema Kitwanga.

See also  Mfahamu Rais Mpya wa Iran Masoud Pezeshkian

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

SERIKALI YAAGIZA MAMLAKA ZOTE KUHUSU UVUNAJI MAJI
HABARI KUU Serikali imeziagiza Mamlaka za Maji kushirikiana na Halmashauri...
Read more
WAZIRI MKUU AONYA MATUMIZI YA BANGI NA...
HABARI KUU Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mbio za Mwenge...
Read more
KATUMBI APINGA USHINDI WA TSHISEKEDI ...
HABARI KUU. Upinzani nchini DRC umewasihi raia kushirikiana nao kupinga...
Read more
Kwanini Yanga ilimhitaji zaidi Chama kuliko Simba?
UCHAMBUZI Faida ya uwepo wa Chama Jangwani kwanza uzoefu wa mashindano...
Read more

Leave a Reply