GODBLESS LEMA ATULIZA UPOTOSHAJI NDANI YA CHADEMA

0:00

HABARI KUU

Aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema ameeleza kuwa hakuna vita ya nafasi ya kugombea Urais ndani ya Chama hicho katika uchaguzi ujao huku akisema amewahi kumsikia Makamu mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu akiweka wazi kuwa hawezi kuchukua fomu ambayo imeguswa na mwenyekiti wake Freeman Mbowe

Kumekuwa na mijadala mitandaoni ikieleza kuwa kuna mvutano wa nani agombee nafasi ya urais ndani ya chama hicho

“Nimeona andiko la BOB Wangwe na maandiko mengine ya watu wengi pamoja na ushauri wake.Jibu langu kwenu ni hili, tukiwa Arusha mahali fulani kwenye mazungumzo yetu ambapo nilikuwepo pamoja na Kamanda Wenje, Heche,Msigwa na Mkti F.Mbowe, Mh Lissu aliongea maneno haya “

“ Nanukuu “ Kaka , Mwenyekiti , ulibeba chupa ya damu nisife wkt nimeshambuliwa kutoka Dodoma ukiwa umesimama kwenye ndege mpaka Nairobi,na ulikaa Nairobi na wenzako hawa muda wote wa matibabu yangu , siwezi kuchukua fomu utakayogusa kwenye Chama hiki,tusiruhusu wapambe watuharibie CHAMA “

“Maneno haya niliyasikia Mimi, Heche, Msigwa, Wenje na Mwenyekiti Mbowe.Hakuna vita kwenye nafasi ya Urais CHADEMA isipokuwa kuna wapambe wajinga na CCM haswa ktk muelekeo wa siasa 2024/2025” ameandika Lema kwenye mitandao ya kijamii .

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

FEISAL ATAJA KUKIMBIWA NA MPENZI WAKE ...
Nyota Wetu Akizungumza na Mwananchi, Mchezaji wa Azam Fc ,Feisal...
Read more
MAHUSIANO YANAJENGWA NA MAMBO HAYA
MASTORI. 1. MAWASILIANO YA WAZI NA HESHIMA. Mawasiliano mazuri ni...
Read more
Rais Jakaya Kikwete kinara wa kutafuta fedha...
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa nafasi yake ya Mwenyekiti...
Read more
FAIDA ZA KULA NDIZI MBIVU KWA MWILI...
AFYA
See also  NPSC Announces Plans to Recruit 25,000 Police Officers Over 5 Years
FAIDA ZA NDIZI MBIVU Ndizi ina aina tatu za...
Read more
KIFAFA CHA MIMBA NI NINI?
Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye...
Read more

Leave a Reply