MASTORI
Naombeni ushauri wenu..
Wake zetu wanatuvua nguo…
Jana ndo niliweza kuthibitisha hili, nilikuwa siamini kabisa…
Nilijaribu kumtongoza shemeji angu mke wa rafiki yangu, na hii ilikuwa mpango wetu mimi na rafiki yangu.
Nakumbuka ilikuwa tar 31 /3/2024 siku ya pasaka, tulitoka out mimi na rafiki yangu.
Tulienda club moja ipo Mbezi Beach – makonde, mida kama saa tatu usiku.
Basi bhana katika kupiga story, rafiki yangu akaanza kuniomba ushauri kuhusu ndoa yake.
Akaniambia kuwa mke wake amebadilika sana, amekuwa na dharau, kiufupi hamsikilizi kabisa.
So rafiki yangu akawa anahisi labda mwanamke kampata mwanaume ambaye anampa kiburi.
Nilimuuliza rafiki yangu Kama amejaribu kuongea na mke wake, na kujua kama kuna shida yoyote..
Akanijibu kuwa ameongea nae mara nyingi, lakini mwanamke anasema hakuna shida yoyote.
Basi bhana tukashauriana, kuwa nijaribu kumtongoza ili kama kuna shida yoyote demu atafunguka.
Basi bhana tar moja nikaenda shopping, nikanunua mazagazaga ya maana, Kisha nikampigia shemu simu…
Nikamuomba tukutane mbali na nyumbani ninamazangumzo nae, tena nikamsisitiza kuwa asimwambie mume wake.
Eebwana eeeh, nilijua atanikatalia, lakini alikubali, nikamtumia location nilipo.
Baada ya lisaa limoja akafika, nikamkaribisha, Kisha nikampatia zile zawadi.
Akafurahi sana, Kisha nikaanza kushusha nyavu zangu, shusha nyavu, shusha nyavu.
Mara akajaa, akaanza kufunguka mwenyewe.
“kiukweli shemeji utakuwa umenisaidia sana make nateseka sana kwenye ndoa yangu,…
Rafiki yako hamna kitu yaani tangu anioe hakuna siku tumefanya round mbili, kila siku round moja tena hata dakika haifiki.
Naomba unipe muda nilifikirie hili kisha nitakupa jibu, si unajua inatakiwa kuwa siri, mume wangu asijue.
Kiukweli ndoa nimeichoka natamani hata kesho anipe talaka.
Ila kwasababu umesema unanipenda Naamini kwako nitapata furaha “
Nyie kumbe ndoa zimebeba mambo mengi sana, mimi nikajua haya mambo ni kwenye video tu kumbe tunaishi nayo.
Jana bhana akanipigia simu, na kunipatia jibu kuwa amenikubali.
Mazungumzo yote nimerecord, Sasa hapa nawaza jinsi ya kumchana mshikaji.
Ni mwambie kuwa anazingua kitandani ndiyo maana mke wake amekuwa na dharau, au ni mwambie shemeji kuwa sipo serious ila nilitaka kujua chanzo cha Ugomvi wao na huu mpango mume wake anaujua.