SAFARI YA ZITTO KABWE KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA HIKO HIVI

0

0:00

HABARI KUU

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu amesema kuwa wao kama Chama katika miaka yao 10 kama Chama chenye usajili wa kudumu, wameweza kujijenga kitaasisi na hivyo wako tayari kuchukua mamlaka ya Nchi Zanzibar na Tanzania bara kwa kumsimamisha Kiongozi wao Mstaafu wa Chama Zitto Kabwe kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jussa ameyasema hayo jana katika sherehe za kitaifa za maadhimisho ya miaka 10 ya ACT yaliyofanyika mkoani Kigoma ambapo amebainisha kuwa Zitto anayo nafasi kubwa ya kukivusha chama hicho na kuchukua uongozi wa Nchi.

ā€œTunajua Mnamtaka Zitto kuwa Mbunge wenu hapa mjini kwenye uchaguzi ujao lakini sisi kama chama tunataka atuvushe kwenye nafasi ya uraisi wa Tanzania kutokana na uwezo na nafasi aliyonayo na tunaomba mtoe baraka zenu kufanikisha hiloā€ ā€”ā€”ā€”Jussa.

Kwa upaande wake kiongozi wa Chama Mstaafu,Zitto Kabwe amesema kuwa ā€œNiko tayari na nimejianda kimaarifa na kusaikolojia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wowote mkinihitaji niko tayari, kuhusu ubunge hakuna shida wakina Nondo wapo na Vijana wengine wakati wowote tupo tayari kuleta mabadiliko ya ya Nchi yetu,mimi ni mstaafu napokea amri kutoka nyie Viongozi wanguā€

Zitto kabwe mbali na hayo amesema miaka 10 ya kuanzishwa kwa Chama hicho inatosha kukifanya kuwa Chama kikubwa Nchini na cha Watu hivyo mpango wa miaka 10 ijayo ni mkakati wa kuhakikisha Chama kinashika dola.

Kuhusu mpango wa Chama kumtaka kugombea Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa 2025, Zitto alisema kuwa alijipanga kugombea Ubunge jimbo la Kigoma Mjini lakini Chama kinayo maamuzi na kama kitaamua hivyo basi hatokuwa na kipingamizi.

See also  WATU ZAIDI YA 100000 WALIVYOKIMBIA VITA DRC
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading