MICHEZO
Mlinzi wa kati Mats Hummels alifunga bao pekee kwa Borussia Dortmund na kuwapa tiketi ya kucheza fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya na kuwaondosha PSG kwa matokeo ya jumla ya 2-0 baada ya mchezo wa kwanza kushinda pia 1-0 walipokuwa nyumbani Signal Iduna Park.
Mara ya mwisho kwa Dortmund kutinga fainali ya michuano hiyo ilikuwa ni miaka 11 iliyopita walipopoteza dhidi ya Bayern Munich kwenye fainali iliyopigwa kwenye dimba la Wembley na sasa wanarejea kujiuliza tena kwenye dimba hilo wakimsubiri mshindi kati ya Real Madrid na Bayern Munich
Beki Mats Hummels na Marco Reus ndiye wachezaji pekee waliokuwepo kwenye kikosi cha Dortmund mara ya mwisho walipocheza fainali ya UCL kwenye uwanja wa Wembley
PSG sasa watalazimika kusubiri kwa msimu mwingine kujaribu tena bahati yao kwenye ligi ya mabingwa Ulaya baada ya mwaka huu kuendeleza jinamizi la kukosa bahati kwani wameacha rekodi ya kuwa timu ambayo mashuti yao yamegonga mwamba mara nyingi zaidi wakifanya hivyo mara 13 msimu huu pekee