MICHEZO
Mapema leo Jumatano (Mei 08) Gazeti la The Sun limeripoti kuwa, Newcastle United wamejipanga kuvuruga mipango ya Manchester United kwa kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini England na klabu ya Crystal Palace Michael Akpovie Olise kwa dau la Pauni Milioni 60.
Olise aliupiga mwingi juzi juzi Jumatatu (Mei 07) katika mchezo dhidi ya Manchester United, na kufunga mabao mawili kati ya manne yaliyopita ushindi klabu hiyo ya Kusini mwa jijini London.
Gazeti la The Sun limeandika: “Manchester United imepata pigo kubwa katika harakati zake za kumsaka Michael Olise,”
“Hiyo ni baada ya Newcastle United kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kumnasa nyota huyo, huku The Magpies kuwa tayari kuliipa Crystal Palace Pauni Milioni 60, ili kumsajili Kiungo huyo mwishoni mwa msimu huu 2023/24.
“Olise alionyesha kwanini Manchester United wanahitaji kumsajili, kwa kuupiga mwingi na kufanikiwa kufunga mabao mawili wakati Palace ikiibanjua United mabao 4-0.
“Wamiliki wenza wa Manchester United ‘Ineos’ wameripotiwa kumfuatilia Olise, huku Sir Jim Ratcliffe akidhaniwa kuwa shabiki wa mchezaji huyo.
“Klabu nyingine inayotajwa kumuwania Olise ni Chelsea, lakini bado Palace inaonekana kuwa na ofa nzuri zaidi.”