MICHEZO
Real Madrid imetinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa jumla wa 4-3 dhidi ya Bayern Munich kwenye nusu fainali.
Mabingwa wa kihistoria wa michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya Real Madrid wamefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo baada ya kuwaondosha Bayern Munich ya Ujerumani kwa kuwalaza 2-1 kwenye mchezo wa marudiano hatua ya nusu fainali
Mwalimu Carlo Ancelotti alimuingiza Joselu dakika ya 81 na mshambuliaji huyo akatumia dakika 3 za mwisho kupachika mabao mawili na kuwapa tiketi ya fainali Real Madrid ambao walikuwa nyuma kwa 1-0 hadi dakika ya 87 baada ya mlinzi Alphonso Davies kuwatanguliza Bayern
Real Madrid sasa watakutana na Borrusia Dortmund kwenye fainali itakayopigwa kwenye dimba la Wembley nchini England
FT: Real Madrid 🇪🇸 2-1 🇩🇪 Bayern Munich (Agg. 4-3)
⚽ Joselu 88’
⚽ Joselu 90 2’
⚽ Davies 68’
Real itachuana na Borussia Dortmund kwenye fainali itakayopigwa Juni 1, 2024 Jijini London katika dimba la Wembley.