Tomas Tuchel akanusha tetesi za kuombwa kusalia Bayern Munich

0:00

MICHEZO

“Imekuwa bahati kuwa hapa, lakini lazima niseme ukweli, kwa sababu tuna makubaliano, hakuna sababu ya kutilia shaka makubaliano haya kwa sasa. Tumefika hapa kwa kushirikiana na Uongozi pamoja na Wachezaji, lakini sina budi kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

“Sihitaji kulazimishwa kuendelea kuwa hapa, wala mimi sitalazimisha kuwa hapa, kilichobaki kwangu kwa sasa ni kuhakikisha naiacha klabu katika mazingira mazuri, tupo kwenye michuano mikubwa Barani Ulaya, nitahakikisha tunapambana ili tuingie Fainali na ikiwezekana kutwaa Ubingwa wa Ulaya.

“Wapinzani wangu (Real Madrid) wapo vizuri hasa wapokuwa katika hatua kama hii tunayokwenda kukutana nao, lakini mchezo bado upo wazi kila mmoja anaweza kushinda na kusonga mbele.”

Swali lingine aliloulizwa Tuchel ni kama ataweza kurejea Chelsea, lakini alijibu: “Nisingependa kujibu lakini sio siri kwamba niliipenda Chelsea, niliipenda Uingereza na niliipenda Ligi ya EPL kwa hakika, ulikuwa wakati wa kipekee sana na ninaukumbuka vizuri sana.” amesema Tuchel

Iwapo Bayern watashinda dhidi ya Real Madrid na kutinga hatua ya Fainali itakayochezwa katika Uwanja wa Wembley, Tuchel atakuwa meneja wa pili kuzipeleka timu tatu tofauti katika Fainali ya UEFA Champions League.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Toni Kroos atangaza kustaafu soka
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading