Mwenyekiti UVCCM Kagera ashinikizwa kujiuzulu kisa hiki

0:00

HABARI KUU

VIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa huo Faris Buruhan kuomba radhi au kujiuzulu kwenye nafasi yake kwa matamshi yake ya hivi karibuni kutaka kuwapoteza watu wanaotukana Viongozi Mitandaoni.

Faris alitoa kauli hiyo hivi karibuni akiwa kwenye ziara katika Mji mdogo wa Rulenge Wilayani ya Ngara mkoani Kagera.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, kijana ambaye ni kada wa Chama hicho Mohamed Ismail, amesema kauli hiyo imewashangaza watu wengi na isipochukuliwa hatua watu wabaya wanaweza kuitumia kuichafua Serikali ambayo haikumtuma kusema maneno hayo.

Amesema Vijana wa mkoa huo wanasikitishwa na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa huo na kwamba wanalaani kauli hiyo inayoleta taswira mbaya na kuwaweka kwenye wakati mgumu vijana wa chama hicho.

Amesema kauli ya Mwenyekiti huyo imekiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 77 inayompa kila mtu haki ya kuishi na kwamba ingawa wanapinga watu wanaotukana mitandaoni lakini si kusema atawapoteza.

Kada mwingine wa chama hicho, Innocent John, alisema hata Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi alikemea kauli hiyo mara tu alipoitoa lakini wanamshangaaa mwenyewe kutojitokeza na kuomba radhi hadharani ingawa muda umepita.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

KELVIN DE BRUYNE KWENYE RADA ZA WAARABU...
MICHEZO Inaripotiwa kuwa klabu ya Al-Nassr kutoka ligi kuu ya...
Read more
5 THINGS TO OFFER YOUR PARTNER ...
❤ What are the things you're supposed to offer your...
Read more
Jurgen Klopp has distanced himself from taking...
Klopp, who left Liverpool at the end of last season...
Read more
Brighton and Nottingham Forest are 𝐒𝐓𝐈𝐋𝐋 unbeaten...
Brighton & Hove Albion and Nottingham Forest maintained unbeaten starts...
Read more
Ancelotti lauds 'rare and extraordinary' Vinicius after...
MADRID, - Real Madrid manager Carlo Ancelotti praised the 'extraordinary'...
Read more

Leave a Reply