0:00
HABARI KUU
Burundi imeishutumu Rwanda kuhusika katika shambulio la guruneti ambalo liliwajeruhi watu 38 karibu na Soko Kuu la zamani mjini Bujumbura.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama Pierre Nkurikiye amefahamisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakipata mafunzo nchini Rwanda kupitia kundi la waasi la Red Tabara ambalo limekuwa liishambulia Burundi.
Amesema kuwa watu sita wamekamatwa Kwa shutuma za kuhusika na shambulio hilo,uchunguzi ukiwa unaendelea kufanyika ili kuwabaini watu wengine.
Hilo linakuwa shambulio la pili baada ya lililotokea maeneo ya Kamenge wiki moja iliyopita na kujeruhi watu sita, mmoja akipoteza maisha baada ya kufikishwa hospitalini.
Related Posts 📫
The teenage sensation signed for the European champions all the...
YOU DON'T APOLOGIZEIf you care about your partner, it will...
Matumizi ya Pombe na Kisukari
Matumizi ya pombe yana athari nyingi...
Celebrated Nigerian artist Onyeka Onwenu,aged 72, tragically collapsed and died...
The President spoke at the Presidential Villa when he received...