RAILA ODINGA ATAJA VIPAUMBELE AKICHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA AU

0:00

HABARI KUU

Kiongozi wa Azimio, Raila Odinga ameeleza majukumu ambayo atatekeleza iwapo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).

Mambo hayo ni pamoja na kuhakikisha AU inafadhili programu na shughuli zake yenyewe.

Odinga pia anaona Afrika inaweza kufanya vizuri zaidi katika kilimo na ndipo anasema atahimiza utoaji wa pembejeo za kilimo zenye ubora wa hali ya juu ili kuongeza uzalishaji maradufu.

Hatua hiyo anasema itaihakikishia Afrika chakula cha kutosha na kukuza biashara ya bidhaa na huduma za kilimo barani Afrika sambamba na kukuza miradi ya kuongeza mnyororo wa thamani ili kuhamasisha na kuongeza thamani ya mauzo ya nje ya ya mazao ya kilimo.

Jambo lingine katika mipango yake akikwaa nafasi hiyo ni kuondoa tatizo la Waafrika wanapotaka kufika katika baadhi ya nchi barani Afrika kulazimika kwenda hadi Ulaya na kisha kurudi maeneo hayo ya Afrika.

“Inasikitisha kwamba miaka 60 ya uhuru, bado kuna maeneo Waafrika wanapaswa kusafiri kwa ndege hadi Ulaya ili kuungana na sehemu fulani za Afrika na kuhitaji pesa nyingi na visa. Hatuwezi kuendelea na hali hiyo.

“Zaidi ya hayo, ni matumaini yangu kuwa nikiwa mwenyekiti wa AUC, nitalisaidia Bara la Afrika kutekeleza ndoto zilizoahirishwa kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kufanya Mto Nile kupitika wote na kuunganisha Bahari ya Atlantiki na Ziwa Victoria hadi Ziwa Tanganyika ili kuongeza ufanisi katika usafiri wa majini,” Raila anasema.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

VITA YA URUSI NA UKRAINE YAMUONDOA KIONGOZI...
HABARI KUU. Kevin Mccarthy anakuwa spika wa kwanza wa Bunge...
Read more
ALEJANDRO GARNACHO NA TEN HAG WAINGIA KWENYE...
MICHEZO
Manchester United wanaamini mshambuliaji kinda wa timu hiyo, Alejandro...
Read more
AS FAR Criticizes Refereeing in Draw Against...
The management of the Royal Armed Forces Sports Association (AS...
Read more
‘I’m no longer motivated by charts, sales’...
American superstar Beyoncé has said she is no longer motivated...
Read more
MILIONI 300 ZAMBAKISHA KIBU DENIS SIMBA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Leave a Reply