MICHEZO
Uongozi wa Klabu ya Bayern Munich inafirikia kumng’oa Kiungo kutoka nchini Ureno Bruno Fernandes kwenye klabu ya Manchester United, ili kuboresha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Ujerumani.
Fikra za kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 zinapewa kipaumbele huko Allianz Arena, kufuatia Man Utd kuwa tayari kupokea ofa.
Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Gazeti la Independent ambalo mapema leo Jumatano (Mei 15) limeripoti kuwa Fernandez yupo tayari kuondoka Old Trafford na kwenda kusaka changamoto mpaya.
Fernandez amekuwa akicheza vyema katika kikosi cha Erik ten Hag msimu huu licha ya United kukabiliwa na uwezekano wa kukosa nafasi ya kucheza Michuano ya Uropa msimu ujao 2024/25.
Gazeti la Independent limeandika: “Bayern Munich inajipanga kumsajili Bruno Fernandes mwishoni mwa msimu huu, Klabu hiyo inaamini kuwa inaweza kumpata kutokana na kuzidi kukasirishwa na Manchester United,”