FAIDA ZA KULA NDIZI MBIVU KWA MWILI WA MWANAMKE

0:00

AFYA

FAIDA ZA NDIZI MBIVU

Ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama Sucrose, Fructose na Glucose na vile vile ina kiasi kingi cha ufumwele (fibre) ambacho husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.
Ndizi ina uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili. Unaweza kupata nishati ya kufanyakazi ya muda wa dakika.
kula ndizi mbili tu.

MFADHAIKO WA AKILI (DEPRESSION)
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama Cha Afya ya Akili cha Taifa (MIND) cha nchini Uingereza, kwa watu wanaosumbuliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili, watu wengi waliondokana na tatizo hilo na kujisikia vizuri baada ya kula ndizi mbivu. Hali hii inatokana na ukweli kwamba ndizi ina kirutubisho kinachojulikana kama tryptophan, ambacho ni aina fulani ya protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.

MATATIZO WAKATI WA HEDHI (PMS)
Kama wewe ni miongoni mwa wale akina mama wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu na unaweza kuponywa. Vitamin B6 iliyomo kwenye ndizi, hurekebisha kiwango cha sukari ambacho huweza kuathiri hali ya mtu.
UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA)
Ndizi ikiwa ni chanzo kizuri cha madini aina ya chuma (iron), inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya upungufu wa damu kwa sababu madini ya chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.

SHINIKIZO LA DAMU
Tunda hili ni la aina ya kipekee, lina kiwango kikubwa cha madini ya potasiamu (potassium) na wakati huo huo lina kiasi kidogo sana cha chumvi (sodium) hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.
Ukweli huo, hivi karibuni umeifanya Mamlaka ya Dawa na Chakula ya nchini Marekani, iwaruhusu wazalishaji na wauzaji wakubwa wa ndizi nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari ya shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.

NGUVU YA AKILI
Hivi karibuni, wanafunzi wapatao 200 wa Shule ya Twickenham nchini Uingereza, walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi mbivu wakati wa mlo wa asubuhi (breakfast), wakati wa mapumziko na wakati wa chakula cha mchana, ndizi ziliongeza uwezo wa akili zao. Utafiti unaonesha kuwa potasiamu iliyojazana kwenye ndizi, ina uwezo wa kumsaidia mwanafunzi kuamsha uwezo wake wa kujisomea.

MZIO (HANGOVER)
Moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unaotokana na ulevi wa jana yake (hangover) ni kunywa ‘Milkshake’ iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali. Ndizi hutuliza tumbo, ikisaidiwa na asali, hurejesha kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu wakati maziwa hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake.
Ndizi pia husaidia katika matatizo mengine kama vile kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kutuliza vidonda vya tumbo, kuondoa asidi tumboni, kushusha joto mwilini, kurekebisha mapigo ya moyo, n.k.
Hivyo ndizi ni tiba ya magonjwa mengi na ni bora. Ukiilinganisha na epo (apple) ndizi ina protini mara nne zaidi, wanga mara mbili, vitamini A na chuma mara tano, na madini mengine mara mbili zaidi ya epo.

See also  JE KUDONDOKA KWA MATITI YA MWANAMKE KUNASABABISHWA NA KUSHIKWASHIKWA NA MWANAUME?

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

DIAMOND PLATINUMZ KWA ORODHA YA WANAWAKE HII...
NYOTA WETU. Toka kwenye uumbaji imeonekana Mwanamke ana nguvu sana...
Read more
Tottenham have completed a £65m deal with...
Tottenham completed the signing of striker Dominic Solanke from Premier...
Read more
Liverpool are reportedly closing in on the...
Liverpool are entering a new era under Slot, who has...
Read more
The Kaduna State House of Assembly says...
The Chairman, Fact-Finding Committee and Deputy Speaker of the State...
Read more
MERCY EKE HOSPITALISED HOURS AFTER PARTYING WITH...
CELEBRITIES Reality TV star, Mercy Eke reflects on life as...
Read more

Leave a Reply