MICHEZO
“Kitendo changu cha kushangilia kilikuwa ni kuzifikishia ujumbe timu kubwa hapa Tanzania ambazo ziliwahi kuniacha na kunikataa kwa madai nimezeeka.”
“Mbali na kuifunga Simba SC nilipanga pia kuzifunga Young Africans ambao walinusurika kidogo sambamba na Azam FC, lakini nimedhamiria kuzifunga siku moja.”
“Hizo timu ziliniacha baadhi na nyingine zikadai mimi mzee lakini nilisema kila nitakapokutana nao nataka kuwafunga ili wajue mimi sio mzee na nikabahatika kuwafunga Simba SC.”
“Young Africans wana bahati sana mechi ya kwanza nilishawafunga waamuzi wakawabeba, nikawakosa mechi ya pili kidogo na bado Azam hapa Tanzania kuna dharau sana watu wakikuzoea.”
“Mimi bado ni mshambuliaji mwenye nguvu nyingi lakini wao wanakuona mzee dawa yao ni kuwafunga na kuwajibu kama vile ili waheshimu wachezaji.”
Mshambuliaji Kagera Sugar – Obrey Chirwa