BULAYA AIKUMBUSHA SERIKALI KULIPA DENI LA BILIONI 18

0:00

HABARI KUU

Mbunge wa Viti maalumu, Ester Bulaya ameikumbusha Serikali kulipa madeni ya Vyombo vya Habari ili viwezi kujiendesha, kauli ambayo inakuja ikiwa wiki moja imepita tangu Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko kuhimiza suala hilo.

Akiongea hii leo Mei 16, 2024 Bungeni Jijini Dodoma Bulaya amesema Serikali inadaiwa zaidi ya bilioni 18 na Vyombo mbalimbali vya Habari ambavyo vinategemea matangazo kutoka serikalini, huku akimuhoji Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kuhusu suala hilo.

Amesema, “wanapolipwa ndio wataanza kulipa mishahara, wataweza kujiendesha na hapo kuna baadhi ya vyombo vingine havijaorodheshwa katika madeni hayo, vyombo vingine binafsi zaidi ya bilioni saba ziko nje hawa watu watafanyaje kazi? Mhe. Nape sasa unadhani kwa madeni sugu hayo unadhani watajiendeshaje.”

Bulaya ameongeza kuwa, “Sisi waandishi wa habari kazi yetu kufanya kazi tu hatuna wa kututetea mpaka ifike leo humu ndani tuanze kuzungumza hii sio Sawa tunaomba hawa watu walipwe, mbona kuna taaluma nyingine hawakopwi, kuna taswira hapa imejengeka kama Wanahabari ni kama watu wamefeli sehemu fulani wamekuja kutafuta ajira, hii siyo.”

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Adebayo feels right at home in Mexico...
MEXICO CITY, - Bam Adebayo won an Olympic gold medal...
Read more
MIAKA 60 YA MAPINDUZI YA KUJIVUNIA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
KOCHA MIGUEL GAMONDI ATAJA ORODHA YA WACHEZAJI...
MICHEZO Taarifa kutoka ndani Young Africans ni kwamba kocha mkuu...
Read more
WHY MEN NEED LOVE AND HELP IN...
LOVE TIPS ❤ MEN NEED LOVE AND HELP TOO...✍️1. MEN...
Read more
WACHEZAJI SIMBA KUPATA KIASI HIKI CHA PESA...
MICHEZO
See also  Mkuu wa Wilaya Morogoro Rebeca Nsemwa ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu Diwani Kata Mwembesongo Mhe.Ally Rashidi Kalungwana Kwa kitendo cha Kutumia vibaya madaraka yake kujenga vibanda vya biashara katika eneo la wazi Soko Kuu la chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro
Wachezaji wa Simba washindwe wao tu sasa hivi hiyo...
Read more

Leave a Reply