HABARI KUU
“JKT TUKO TAYARI KUTEKELEZA, MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA”
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema kuwa wapo asilimia 98 ya kuhakikisha kwamba matumizi ya Nishati ya Kuni na Mkaa yanapotea ndani ya Jeshi lao la JKT
Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika kikosi Cha Jeshi 822 Rwamkoma JKT Kilichopo Wilayani Butiama Mkoani Mara
Meja Jenerali Mabele amesema kuwa Serikali inapotoa maelekezo wao kama Jeshi wanakuwa watu wa kwanza kuyatekeleza maagizo hayo na wapo tayari wakati wote Kwa ajili ya maelekezo
Meja Jenerali Mabeyo ameongeza Kwa kusema kuwa tangu Serikali walipoanza kuzungumza kuhusu matumizi ya Nishati safi ya Kupikia wao waliona ni maagizo na hata kabla ya maelekezo hayajatolewa wao walishaanza kuyafanyia kazi kutokana huo ndio utaratibu wao wa maisha
Kwa upande wake Kamanda Kikosi Cha Rwamkoma JKT Luteni Kanali Gaudencia Mapunda amesema kuwa manufaa wanayoyapata katika matumizi ya Nishati safi ya Kupikia ni utunzaji wa Muda na hata vijana wanaopika katika majiko hayo hawaathiriki na Moshi tofauti na kipindi Cha nyuma wakati walipokuwa wakitumia Nishati chafu ya Kupikia.