0:00
NYOTA WETU
Matokeo ya uchunguzi wa mwili wa marehemu mwimbaji, Ilerioluwa Aloba, almaarufu Mohbad yametoka.
Kwa mujibu wa ripoti inadai kuwa wataalamu wameshindwa kubaini sababu ya kifo cha mwanamuziki huyo kwasababu mwili uliofanyiwa uchunguzi ulikuwa umeharibika sana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana May 15,2024 Wakili Mkuu wa Serikali nchini Nigeria Wahab Shittu amesema kuwa “uchunguzi uliofanywa na madaktari unadai kuwa wameshindwa kujua sababu ya kifo cha mwanamuziki huyo kwani wakati vipimo vinafanyika mwili wake ulikuwa umeharibika sana’.
Mohbad alifariki dunia September 12,2023 kifo chake kilikuwa na utata ambao ulipelekea mwanamuziki Naira Marley kukamatwa kwa kutuhumiwa kuhusika na kifo hicho.
Related Posts 📫
“Marrying a pastor was the biggest mistake of my life,”–Kumawood...
HOT NEWS
Bill Gates former spouse,Melinda French Gates, will receive...
NYOTA WETU.
Mwigizaji Lupita Nyong'o ametangaza kuachana na Selema Masekela...
OUR STAR 🌟
Nigerian singer, songwriter, and record producer Damini...