MICHEZO
Ashley Cole ameripotiwa kuwekwa kwenye mipango ya kupewa kazi ya ukocha.
Beki huyo wa zamani wa England mwenye umri wa miaka 43, alifurahia maisha yake matata sana kwenye kipindi chake alichokuwa mchezaji kabla ya sasa kuingia kwenye ukocha.
Aliwahi kufanya kazi chini ya Frank Lampard na Wayne Rooney huko Birmingham.
Cole amebaki kwenye kikosi hicho cha The Blues baada ya Rooney kufutwa kazi baada ya kuiongoza timu hiyo kwenye mechi l5.
Lakini, kwa sasa staa huyo wa zamani wa Chelsea huenda akakabidhiwa kazi ya kwanza ya kuwa kocha mkuu baada ya klabu kadhaa huko kwenye Championship wakitaka kumpa kazi.
Cole amekuwa na uzoefu mkubwa wa mambo yanavyokwenda kwenye Championship baada ya kuwa huko Birmingham na alikuwa kocha wa Derby kati ya 2018 na 2019.
Baadae aliondoka kumfuata Lampard huko Chelsea kwenda kuwa kocha kwenye kikosi cha kwanza na mwanzo alikuwa akifanya kazi kwenye akademia ya klabu hiyo ya Ligi Kuu England.
Cole alifanya kazi na Lampard pia huko Everton, lakini mafanikio yake nakubwa alipata kwenye kikosi cha vijana cha England chini ya miaka 21, alipoisaidia kushinda ubingwa wa Ulaya mwaka jana, ilipokuwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 40.