VITA YA BANDARI ZA DAR NA MOMBASA YAMPELEKA RUTO KWA MUSEVENI

0:00

HABARI KUU

Rais wa Kenya, William Ruto na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Museveni wametia saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano, ikiwemo usafirishaji wa mafuta ya Petroli kutoka Kampala kupitia Bandari ya Kenya.

Utiaji wa saini huo, hautaathiri mpango wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka mjini Eldoret katika mkoa wa bonde la ufa nchini, Kenya hadi Uganda.

Ziara hiyo inafuatia kikao cha pili cha Tume ya Pamoja ya Mawaziri (JMC) kilichomalizika hivi karibuni kati ya Kenya na Uganda, ambapo mikataba saba ya makubaliano (MoU), ilisainiwa ikiwemo utumishi wa umma, elimu, maendeleo ya biashara ndogo ndogo, michezo, masuala ya vijana, biashara na uwekezaji.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Kenya, Musalia Mudavadi amesema ziara ya rais Museveni ni muhimu ikilenga kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Kwanini Daraja la Magufuli (Kigongo-Busisi) limechelewa kutumika...
Daraja la John Magufuli (Kigongo- Busisi) lenye urefu wa...
Read more
Lands Cabinet Secretary Nominee Wahome Touts Wealth,...
The Lands Cabinet Secretary nominee, Alice Wahome has appeared before...
Read more
MWENYE SEHEMU ZA SIRI MBILI AONDOLEWA UKE...
HABARI KUU Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke imefanyia...
Read more
RUBANI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI 10 KWA...
HABARI KUU Rubani mmoja wa Shirika la Ndege la Delta,...
Read more
YOUNG AFRICANS YATAJA SABABU ZA KUMUACHA JOYCE...
MICHEZO Wakati Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans wakisaka...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Sababu Zinazochangia Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

Leave a Reply