MICHEZO
YOUNG AFRICANS KAZI KWENU SASA.
Tunafahamu kuwa klabu ya Yanga kwa kipindi kirefu imekuwa ikimuhitaji Winga raia wa Congo DR anayekipiga ndani klab ya Tp Mazembe Phillipe Kinzumbi (24), Kama ilivyo kwa klab ya Tp Mazembe imekuwa ikimuhitaji sana Mshambuliaji huyo raia wa Zambia tangu akiwa ligi kuu ya Zambia kabla ya kuwahiwa na Young Africans,
Taarifa Njema kwa Wananchi ni kwamba Wamefikia pazuri kimazungumzo baina ya Kinzumbi na Uongozi wa Young Africans kwanza,
Uongozi wa klab ya TP Mazembe sasa Umeuambia Uongozi wa klab ya Yanga kufanya Swap deal kwa maana kuwaachia winga wao tegemeo Phillipe Kinzumbi, Wakimaanidha kuwa Young Africans wao watatoa Musonda + pesa kiasi waende TP Mazembe na Phillipe Kinzumbi aende Yanga SC Mwishoni Mwa msimu huu,
Mchezaji (Kinzumbi) yuko tayari kujiunga na mabingwa mara 30 wa Tanzania Yanga SC.