Serikali kuja na mpango huu wa usimamizi wa fedha za mikopo

0

0:00

HABARI KUU

Serikali ipo katika maandalizi ya usimami wa mikopo ya asilimia 10 kwa kuamua kuanzisha kitengo maalumu cha usimamizi wa Mikopo hiyo kwa ngazi ya Wizara, na kamati ya usimamizi wa mikopo katikati ngazi ya Mikoa, Halmashauri na Kata.

Ameyasema hayo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ā€“ TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Zainabu Katimba Bungeni Jijini Dodoma hii leo Mei 17, 2024 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Christina Christipher Mnzava.

Mnzava alitaka kujua je, Serikali imejipanga vipi katika usimamizi wa mikopo ya asilimia 10, pindi itakapoanza kutolewa tena kuanzia Julai mosi?

Akijibu swahi hilo, Katimba amesema, ā€œtimu iliundwa kufanya mapitio na kuhakikisha unatengenezwa utaratibu bora zaidi kwa ajili ya kuhakikisha Mikopo, hii inatoka na inaenda kuwanufaisha walengwa na tayari katika Muundo wa usimamizi wa mikopo hii.

Amesema”kutaanzishwa Kitengo cha usimamizi wa Mikopo katika ngazi ya Wizara Ofisi ya Rais TAMISEMI na kamati za usimamzizi wa Mikopo katika ngazi ya Mikoa, Halmashauri na Kata, mikopo hii inayotokana na Mapato ya ndani ya Halmashuri, ilisitishwa kutokana na maelekezo ya Serikali ya kuangalia upya utaratibu na changamoto zilizokuwepo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Cardiff City defender Perry Ng has moved a step closer to playing for Singapore after training with their national squad this week.
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading