PAUL MAKONDA AMUWEKA KITIMOTO MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA

0:00

HABARI KUU

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha kuanza uchunguzi dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Eng. Juma Hamsini na baadhi ya wasaidizi wake kutokana na tuhuma za Rushwa na ubadhirifu wa fedha za walipa kodi zinazowakabili.

Akizungumza na wadau wa utalii mkoani humo leo, Makonda amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Missaile Mussa kuwasimamisha kazi watumishi wote waliotajwa kuhusika na tuhuma hizo ili kupisha uchunguzi.

Hatua hio imefuata baada ya Mwenyekiti wa waongoza watalii Mkoa wa Arusha, Wilbard Chambulo kudai kuwa baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wamekuwa wakitengeneza nyaraka bandia pamoja na kuchepusha baadhi ya makusanyo ya kodi zinazotokana na sekta ya Utalii.

Chambulo amemweleza Mkuu wa Mkoa kwamba watumishi hao wamekuwa na makampuni hewa ya utalii pamoja na kuwa na namba tofauti za ulipaji wa kodi na usajili hewa wa makampuni yenye kufanana na makampuni halisi ya utalii yalipo ndani ya Jiji la Arusha.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

NDEGE MPYA YA BOEING KUPOKELEWA MACHI 26...
HABARI KUU Shirika la ndege la Tanzania, Air Tanzania ...
Read more
Djokovic withdraws from Paris Masters
Novak Djokovic has withdrawn from the Paris Masters, both he...
Read more
Chelsea hold on to beat Leicester despite...
Goals from Nicolas Jackson and Enzo Fernandez helped Chelsea to...
Read more
Former world number one Naomi Osaka says...
Japan's Osaka returned to the WTA Tour in January after...
Read more
Bad signings, no identity and big losses:...
Erik ten Hag’s 2 1/2-year tenure at Manchester United will...
Read more
See also  TUNDU LISSU AHOFIA USALAMA WAKE ATOA AHADI YA KUWATAJA WANAOMFATILIA

Leave a Reply