MICHEZO
Kocha wa klabu ya Brighton ya Ligi kuu England, Roberto De Zerbi ataondoka klabuni hapo baada ya mchezo wa klabu hiyo wa kufunga pazia la Ligi hiyo dhidi ya Manchester United siku ya Jumapili Mei 19, 2024.
De Zerbi anakuwa kocha wa tatu wa Ligi Kuu England ambao michezo ya kesho ya kufunga pazia la Ligi kuu England msimu wa 2023/24 itakuwa mechi zao za mwisho kutumikia vilabu vyao baada ya Jurgen Klopp na Liverpool na David Moyes wa West Ham United ambao pia wameaga.
De Zerbi alichukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo almaarufu ‘Seagulls’ katikati ya msimu wa 2022/23 akichukua mikoba ya Graham Potter aliyetimkia Chelsea kwa wakati huo.
De Zerbi aliiongoza klabu hiyo kucheza Ligi ya Europa katika msimu wake wa kwanza baada ya kumaliza ligi katika nafasi ya sita.