JESHI LAZIMA JARIBIO LA MAPINDUZI DRC

0:00

HABARI KUU

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limetangaza kuzuia jaribio la mapinduzi dhidi ya Rais Felix Tshisekedi huko Kinshasa.

Hayo yamebainishwa na Msemaji wa jeshi la DR Congo Brig Jenerali Sylavin Ekenge katika kituo cha runinga cha taifa RTNC TV ambapo amesema kuwa washukiwa kadhaa wamezuiliwa na “hali sasa imedhibitiwa”.

Tangazo hilo linajiri saa chache baada ya watu wenye silaha kushambulia nyumba ya Vital Kamerhe ambaye ni mkuu wa zamani wa majeshi na mshirika wa karibu wa Rais Felix Tshisekedi.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kundi la watu takriban 20 wakiwa wamevalia sare za jeshi walishambulia makazi hayo na ufyatulianaji wa risasi ukafuatia.

Rais Tshisekedi hajatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo.

Wakati huo Balozi wa Japani katika mji mkuu wa Congo amewaonya wajapani walioko DRC kutotoka nje.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WANAJESHI WATATU WA TANZANIA WAUAWA KWENYE MAPIGANO...
HABARI KUU Wanajeshi watatu wa Tanzania wanaohudumu katika kikosi cha...
Read more
Three Chibok girls in 2014 earned University...
HARD NEWS Three of the Chibok girls who fled from...
Read more
JOAN LAPORTA ANAMTAKA XAVI HERNANDEZ KUENDELEA KUWA...
MICHEZO Rais wa FC Barcelona, Joan Laporta amesisitiza kwamba anataka...
Read more
FAHAMU KUHUSU ULINZI WA RAIS WA MAREKANI...
MAKALA Unaweza kujiuliza Taifa kubwa ambalo limewahi kuwashuhudia maraisi wake...
Read more
ROBERTO DE ZERBI KUMRITHI TUCHEL BAYERN MUNICH...
MICHEZO Kocha wa klabu ya Brighton, Roberto De Zerbi yupo...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania(TALGWU),kimemjia juu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda juu ya matamshi aliyoyatoa dhidi ya Mtumishi wa umma wilayani Longido, kikidai kitendo hicho kinavunja heshima ya mfanyakazi,Kudhalilisha na kuvunja hali na morali ya kufanya kazi.

Leave a Reply