Israel ilivyohusika kwenye kifo cha Rais wa Iran Ibrahim Raisi

0:00

HABARI KUU

Rais wa Iran Ibrahim Raisi (63), Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo, Amir Abdollahian na Maafisa wengine saba waliokuwamo kwenye msafara wamepatikana wakiwa wamefariki katika eneo la ajali ya Helikopta iliyoanguka katika eneo la Jolfa, lililopo zaidi ya kilomita 600 kutoka Tehran karibu na mpaka wa jimbo la kaskazini-magharibi mwa Azerbaijan wakati wakitokea katika mkutano na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Iran la Mehr la Nchini Iran, limeripoti kuwa, Helikopta hiyo ilitoweka kwenye rada Jumapili mchana na katika ajali hiyo hakuna mtu aliyenusurika na Serikali ya Iran bado haijatia neno kuhusiana na tukio hilo

Mkuu wa shirika la Hilali Nyekundu la Irani, Pirhossein Koolivand amesema timu za waokoaji ziliyafikia mabaki ya helikopta hiyo na kudai kuwa hali mbaya ya hewa ilichangia kutatiza shughuli za uokozi.

Nchi kadhaa zikiwemo Urusi na Uturuki zimetoa msaada katika operesheni ya uokoaji, huku ndege isiyo na rubani ya Uturuki pia ikiruka katika anga ya Iran kusaidia shughuli ya utafutaji, huku Kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei akitoa wito kwa Wairan kumwombea Raisi.

Raisi ambaye alizaliwa mwaka wa 1960 huko Mashhad, kaskazini-mashariki mwa Iran, aliapishwa kuwa rais mpya wa Iran Agosti 2021 na alishinda uchaguzi wa urais chini ya asilimia 62 ya kura kama mgombea mkuu wa vyama vya siasa kali na anayependwa zaidi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa katiba ya Iran, Raisi alikuwa ni Kiongozi wa pili kinyadhifa, chini ya Khamenei ambaye ni Mkuu wa nchi na pia ndiye mwenye uamuzi wa mwisho katika masuala yote ya kimkakati na tayari Baraza la Mawaziri limefanya kikao na kudai litaujulisha umma kuhusu wakati na mahali itakapofanyika shughuli ya kuaga mwili wa Rais Raisi.

See also  Liverpool forward Darwin Nunez has been banned for five international games for an altercation with spectators after his national team Uruguay were beaten by Colombia.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

YANGA YARUDI PALE PALE ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
Read more
President Ruto Nominates Second Wave of Cabinet...
President William Ruto has nominated a second group of Cabinet...
Read more
FAIDA NA HASARA ZA KUPEKUA SIMU KWA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Danny Welbeck's goal secured victory for Brighton...
Danny Welbeck's first-half goal against the run of play gave...
Read more
HOW NOT TO TALK TO YOUR SPOUSE
Don't order your spouse around like a servant. It shows...
Read more

Leave a Reply