MAKALA
Imethibitika kwamba Rais wa Iran amefariki katika ajali iliyotokea jana. Mwenyekiti wa “Red Crescent” Iran, Kolivand, ametangaza kuwa mabaki ya helikopta iliyokuwa imembemba Rais Ebrahim Raisi na maafisa wengine kadhaa yamepatikana.
Mabaki ya helkopta hiyo yamepatikana Masaa nane tangu kuripotiwa kutikea kwa ajali hiyo ambapo wataalamu wa uokozi wakisema hali mbaya ya hewa ndio chanzo cha ajali hiyo.
Kwamjibu wa wataalamu wa masuala ya anga, Helikopta hiyo ilipatikana kaskazini magharibi kwenye mlima ya wastani katika eneo la Varzaghan, kijiji cha Uzi katika misitu ya Arsbaran kutokana na ukungu mkubwa.
Orodha ya Abiria waliokuwa kwenye helikopta hiyo ni pamoja na:
1. Rais wa Iran, Ibrahim Raisi
2. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir Abdollahyan
3. Ayatollah Al-Hashemi, Imamu wa Msikiti wa Tabriz
4. Gavana wa Mkoa wa Azabajani Mashariki, Malik Rahmati
Mitazamo ya Wadadisi wa mambo inachukulia kwamba tukio hili linahusisha uhasama uliopo kati ya Tehran na Tel Aviv, na kwamba Mossad imehusika katika ajali hiyo, Lakini mapema jana baada ya tukio hili, Tel Aviv ilikanusha kuhusika na tukio hili, Hata hivyo ni vigumu kuamini kanusho lao kwa uzoefu wa matukio ya kiajali eneo la mashariki ya kati, Mengi ya matukio huwa ni ya kutengenezwa.
Kwa vyovyote vile, kuna sababu nyingi zinazotilia shaka ajali hii kwani katika msafara wa Rais wa Iran kulikuwa na Helkopta tatu ambapo mbili zimetua salama licha ya hali mbaya ya hewa, lakini iliyombeba Rais ikachepuka njia na kupeperushwa mbali sana kiasi cha kuchukua masaa nane kuja kuipata katika milima na misitu mikubwa, na mwili wa Rais haujapatikana kutokana na sehemu kubwa ya mabaki ya helkopta hiyo kuungua.