NYOTA WETU
Kwa mujibu wa mtandao wa Wealth, hawa ndio Mabilionea wenye umri mdogo zaidi duniani (pangusa kushoto kuona orodha kamili).
Katika orodha hii, Bilionea mwenye umri mkubwa zaidi ni Ben Francis na Mark Mateschitz wakiwa na umri wa miaka 31, na mdogo zaidi akiwa ni Clemente Del Vecchio mwenye umri wa miaka 19.
Tajiri zaidi kati yao ni Mark Mateschitz mwenye utajiri wa kushangaza wa dola Bilioni 39.6 za Kimarekani, wakati tajiri mdogo zaidi ni Ben Francis ambaye anajivunia utajiri wa kushangaza wa dola Bilioni 1.3 za Kimarekani.
Orodha hii inajumuisha watu watatu wa familia ya Del Vecchio ambao ni Leonardo Maria, Clemente na mwingine ambaye hajatajwa jina ambapo utajiri wa familia hiyo unatokana na umiliki wao wa kampuni kubwa ya Luxottica.