YANGA KUTUMIA UWANJA WA MKAPA KWENYE SHEREHE ZA UBINGWA

0:00

MICHEZO

Klabu ya Yanga SC imekubaliwa kuutumia uwanja wa Mkapa katika sherehe zao za Ubingwa wa (30) wa ligi kuu Tanzania bara.

“Tulipeleka Maombi yetu Bodi ya Ligi na kwa Serikali tukitaka Mechi yetu dhidi ya Tabora United tukabidhiwe kombe letu, sasa ni Rasmi Yanga tutakabidhiwa kombe letu Jumamosi, Mei 25, mechi hii itapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa,”

“PARADE LA UBINGWA Mwaka huu ni Mei 25, 2024 kuanzia saa 5 asubuh palepale Benjamin Mkapa na baada ya mechi tutatoka Kwa Mkapa hadi Kurasini Uhasibu, Mtoni, Temeke Mwisho, Mwembe Yanga, Vetenari, Tazara, Buguruni huku mjini mnaelewe njia haina haja ya kueleza na Safari hii hatupiti tu tutakaa kidogo,”

“Mchezo wa kukabidhiwa ubingwa dhidi ya Tabora United Tiketi za VIP A hazitapatikana tayari zimeshakuwa Sold Out, VIP B ni Tsh. 10,000, VIP C Tsh. 5,000 alafu mzunguko kiIngilio ni Buku ya ubingwa,”

“Kesho tunasafiri majira ya saa nne asubuhi kuelekea pale mkoani Dodoma kucheza dhidi ya Dodoma Jiji. Mchezo huo utafanyika tarehe 22 Mei 2024. Mechi hii ya Dodoma tumeifanya mechi ya kushukuru benchi la ufundi. Hivyo itakuwa ni 𝐆𝐀𝐌𝐎𝐍𝐃𝐈 𝐃𝐀𝐘

Kwenye 𝐆𝐀𝐌𝐎𝐍𝐃𝐈 𝐃𝐀𝐘 itakapofika 𝐝𝐚𝐤𝐢𝐤𝐚 𝐲𝐚 𝟑𝟎, wana Yanga wote tunapaswa kusimama kumpigia makofi 𝐆𝐚𝐦𝐨𝐧𝐝𝐢 na benchi lake la ufundi kwa dakika moja. Tunampa heshima 𝐆𝐚𝐦𝐨𝐧𝐝𝐢 kwa kutupatia uingwa wa kishitoria mara ya (30)”

Ameyasema hayo, Ally Kamwe ,Afisa habari na Mawasiliano wa timu hiyo ya Yanga.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Senegalese government issues firm ultimatum to the...
In a groundbreaking initiative four years back, Senegal allocated land...
Read more
Tabby Brown, model and ex- football star...
Ex- Chelsea and Arsenal star Model Tabby Brown, passed away...
Read more
HOW TO KNOW IF THE LOVE IS...
LOVE TIPS ❤
See also  PACOME, AUCHO NA YAO WAONGOZANA NA YANGA KUIFUATA MAMELODI
When someone loves you, you know and...
Read more
Singer Rema allegedly given N4.5 billion ($3...
Nigerian artist Rema is all set to grace the extravagant...
Read more
ABIRIA WALIVYOKWEPA VIFO,LORI NA MABASI YAKIGONGANA ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Leave a Reply