Wairan waandamana kuomboleza kifo cha Ebrahim Raisi

0:00

HABARI KUU

Maelfu ya watu wamekusanyika katikati mwa mji mkuu wa jimbo la Azerbaijan Mashariki, wakiomboleza huku wakiwa wamebeba picha za aliyekuwa rais wa Iran, Ebrahim Raisi aliyefariki katika ajali ajali ya Helikopta.

Katika ajali hiyo, Ebrahim Raisi (63), aliaga dunia sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo, Amir Abdollahian na Maafisa wengine saba wa Serikali.

Mwili wa Raisi, Waziri wake wa Mambo ya Nje na watu wengine waliokuwemo kwenye helikopta hiyo yatapelekwa Qom kisha jijini Tehran ambapo kutakuwa na utoaji wa heshima za mwisho.

Kiongozi Mkuu wa Taifa hilo, Ayatollah Ali Khamenei atatangaza sala ya mazishi ambapo waumini wataungana na Viongozi wa kigeni ili kushiriki zoezi hilo muhimu.

Taarifa za Waislamu wengi wa Kishia nchini Iran, wanasema mwili wa Rais utapelekwa Mashhaa, eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kwa ajili ya mazishi, kwenye kaburi la Imam Reza, mrithi wa nane wa Mtume Muhammad.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

ISRAEL YAOMBWA KUTOKULIPA KISASI
HABARI KUU Waziri wa mambo ya nchi za nje wa...
Read more
Newcastle United kutibua mpango wa Manchester United...
MICHEZO Mapema leo Jumatano (Mei 08) Gazeti la The Sun...
Read more
CHRISTOPH BAUMGARTNER AWEKA REKODI HII
NYOTA WETU Kiungo Christoph Baumgartner wa Austria jana alifunga bao...
Read more
CARLO ANCELOTTI AKIRI NI VIGUMU KUMUACHA LUKA...
MICHEZO Kocha Mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti amekiri ni...
Read more
Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain...
Inaelezwa kuwa, mabosi wa PSG wanataka kumchukua fundi huyu ikiwa...
Read more
See also  WHO IS THOMAS FULLER "Negro Tom" and the "Virginia Calculator "

Leave a Reply