Ayatollah Ali Khamenei azidiwa na huzuni akimuaga Ebrahim Raisi

0:00

HABARI KUU

Kiongozi wa juu nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei ameonekana kuzidiwa na huzuni na kuamua kuondoka baada ya kuongoza ibada ya sala ya kuaga miili ya aliyekuwa Rais wa taifa hilo Ebrahim Raisi na maafisa wengine waliokufa kwenye ajali ya helikopta, zoezi lililoshuhudiwa na maafisa wa ngazi za juu zaidi ya 40 kutoka mataifa ya kigeni mjini Tehran.

Khamenei ameongoza shughuli hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Tehran, ambapo vilio vilisikika kutoka kwa waombolezaji waliokusanyika kwa ajili ya kuwaaga viongozi wao, wakati majeneza yao yaliyokuwa yamezungushiwa bendera ya Iran, yalipopangwa mbele ya maafisa wandamizi.

Khamenei aliongozwa ibada hiyo akitumia kitabu kitakatifu cha Kiislamu cha Quran na aliondoka mara baada ya sala ambapo wakati wote Rais wa mpito wa Iran, Mohammad Mokhber alikuwa amesimama karibu na Khamenei akionekana kububujikwa na machozi.

Miongoni mwa waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Maafisa waandamizi wa Kikosi cha Walinzi wa Kimapinduzi, chenye ushawishi mkubwa nchini humo, akiwemo Kiongozi wa Wanamgambo wa Hamas wa Palestina, Ismail Haniyeh.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MANCHESTER United resume their Premier League title...
The Red Devils won their opening match and then lost...
Read more
ISRAEL YASHITAKIWA MAHAKAMA KUU YA UMOJA WA...
HABARI KUU Mahakama Kuu ya Umoja wa Mataifa leo Jumatatu...
Read more
SABABU AL-HILAL OMDURMAN KUJIUNGA NA LIGI KUU...
MICHEZO Mkurungezi wa Bodi ya Ligi , Almas Kasongo amekiri...
Read more
Kenyan Government Raises Concerns Over Ford Foundation...
The Kenyan government has written to the Ford Foundation, expressing...
Read more
HOW NOT TO TALK TO YOUR SPOUSE
Don't order your spouse around like a servant. It shows...
Read more
See also  Amuua Rafiki Yake Kisa Milioni 61

Leave a Reply