MICHEZO
Uongozi wa Klabu ya Chelsea umetangaza kuachana na Kocha Mauricio Roberto Pochettino Trossero kwa makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja Mkataba ambao ulisainiwa mapema msimu wa 2023/24.
Kocha huyo alisaini mkataba wa miaka miwili, hivyo sehemu ya mwaka mmoja katika Mkataba wake ndio imevunjwa kwa makubaliano maalum yaliyofikia kati yake na Uongozi wa juu wa Chelsea.
Akizungumzia kuhusu kuondoka katika klabu hiyo, Pochettino amesema:
“Sina budi kuushukuru Uongozi wa Chelsea kwa nafasi kubwa waliyonipa, nimekuwa sehemu ya historia ya Klabu hii,”
“Pia ninawashukuru sana Wachezaji wangu na Mashabiki ambao siku zote tulikuwa pamoja katika kipindi cha Raha na Simanzi, ninaitakia kila la kheri Chelsea katika mpango wake mpya.”
“Ninajivunia kuiacha klabu katika nafasi nzuri, Msimu ujao itashiriki Michuano ya Ulaya, hii imetokana na kazi kubwa niliyoifanya kwa kushirikiana na Wachezaji wangu hadi siku ya mwisho ya msimu, ninawapongeza sana kwa hilo.”
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.