MICHEZO
Kocha wa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City Pep Guardiola ametajwa kuwa Kocha Bora wa Msimu wa 2023/24 kwenye Ligi Kuu ya England.
Guardiola aliiongoza Manchester City kutwaa taji la nne mfululizo la Ligi Kuu ta England mwishoni mwa juma lililopita, kwa kuifunga West Ham Utd mabao 3-1, Uwanja wa Etihad mjini Manchester.
“Ni heshima kutajwa kuwa Kocha Bora wa Ligi Kuu ya England. Tuzo hii inaonyesha bidii na ubora wa watu katika Klabu na idara zote. Ninajivunia kuwa meneja wa Kundi la Wachezaji wangu na kufanya kazi pamoja na Makocha mahiri na Wafanyikazi wa klabu.
“Kushinda mataji manne mfululizo ni mojawapo ya mafanikio ya kujivunia katika taaluma yangu. Hii ni ligi ngumu zaidi duniani na washindani wetu wamecheza soka la ajabu. Nilipowasili England, sikuwahi kufikiria kuwa pamoja tunaweza kushinda Ligi Kuu mara sita ndani ya miaka saba.
“Tumefanya kitu kisichoaminika na kusherehekea na mashabiki wetu, Jumapili iliyopita ilikuwa siku ambayo nitaikumbuka daima.”