HABARI KUU
Waziri Mkuu wa Chad, Succès Masra, amewasilisha barua yake ya kujiuzulu Mei 22,2024 ikiwa ni zaidi ya wiki mbili baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Rais wa Mei 6 huku Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno, akiibuka mshindi.
“Nimewasilisha kujiuzulu kwangu na kwa Serikali ya mpito, ambayo imekuwa haina umuhimu na kumalizika kwa Uchaguzi wa Rais, na kwa mujibu wa Katiba”, anaandika Succès Masra kwenye ukurasa wake wa Facebook, katika ujumbe uliothibitishwa na Bunge”.
Hili si jambo la kushangaza hata kidogo, kwani hatambui matokeo ya uchaguzi wa Urais.
Kama Mawaziri Wakuu wote wa zamani, anaalikwa kesho kwa kuapishwa kwa Mahamat Idriss Déby, lakini hatarajiwi kuhudhuria.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.