Jacob Zuma awalalamikia majaji kumzuia kugombea Ubunge

0:00

4 / 100

HABARI KUU

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amewalalamikia majaji waliotoa uamuzi wa kumzuia kuwania ubunge katika hukumu walioitoa Jumatatu.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu mahakama kumpiga stop kugombea, Zuma ameiambia BBC kwamba Mahakama ya Kikatiba ilikosea kutoa uamuzi kwamba hafai kugombea, kutokana na hukumu dhidi yake ya mwaka 2021 iliyomwona ana hatia ya kudharau mahakama.

“Nilitarajia hilo kutoka kwa majaji, lakini kwa hakika hawako sahihi hata kidogo,” mzee huyo wa miaka 82 amesema, akisisitiza kwamba katiba inapaswa kubadilishwa.

Kabla ya uchaguzi mkuu wa wiki ijayo, Zuma alikuwa akifanya kampeni chini ya bendera ya chama kipya kilichoundwa cha Umkhonto weSizwe .

Alijiunga na chama hicho baada ya kutofautiana na chama tawala cha African National Congress (ANC), alichowahi kukiongoza.

Tume ya Uchaguzi nchini humo ilisema kuwa katiba inamzuia mtu yeyote ambaye alihukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi 12 kuhudumu kama Mbunge, ujumbe ulioungwa mkono na Majaji wa Mahakama ya kikatiba.

Zuma alipatikana na hatia mwaka 2021 kwa kukataa kutoa ushahidi wake kwenye uchunguzi wa ufisadi wakati wa uongozi wake.

Mawakili wake walikuwa wamesisitiza kuwa ana haki ya kuwa mbunge kwani kifungo chake kilipunguzwa hadi miezi mitatu baada ya Rais wa sasa, Cyril Ramaphosa kumwachia kutoka gerezani kwa kile kilichoonekana kuwa ni jaribio la kuwatuliza wafuasi wa rais huyo wa zamani waliokuwa na hasira.

“Majaji wa Mahakama ya Kikatiba wamenifanyia mzaha sana. Hawazingatii matakwa ya watu wa nchi hii, wanatumia mapenzi yao wenyewe,”

amelalamika Zuma.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  NDEGE ILIYOMBEBA MAKAMU WA RAIS YAPOTEA

Related News 📫

Luis Enrique calls for persistence after PSG's...
PARIS, - Paris St Germain manager Luis Enrique lamented his...
Read more
HOW TO MAKE YOUR CHICKENS GROW BIG...
Every poultry farmer knows that Buyers want BIG chickens. If you...
Read more
Graham out but Scotland boosted by Kinghorn,...
EDINBURGH, - Scotland winger Darcy Graham has been ruled out...
Read more
KELVIN DE BRUYNE KWENYE RADA ZA WAARABU...
MICHEZO Inaripotiwa kuwa klabu ya Al-Nassr kutoka ligi kuu ya...
Read more

Leave a Reply