MICHEZO
Nyota wa klabu ya West Ham United, Lucas Paquetá ameshtakiwa na Chama cha Soka England (FA) kwa utovu wa nidhamu kuhusiana na madai ya ukiukaji wa Kanuni za FA E5 na F3.
“Inadaiwa kuwa Lucas alitaka kuathiri moja kwa moja maendeleo, mwenendo au matokeo kwenye mechi hizi kwa kutaka kwa makusudi kupokea kadi kutoka kwa mwamuzi kwa madhumuni yasiyofaa ya kuathiri soko la kamari ili mtu mmoja au zaidi wanufaike na kamari.
Paquetá (26) raia wa Brazil pia ameshtakiwa kwa ukiukaji mara mbili wa Kanuni ya F3 ya FA kuhusiana na madai ya kushindwa kutii Sheria ya FA F2.
Katika taarifa yake Paquetá amesema : “Nilishangaa na kufadhaika sana kuona kwamba FA wameamua kunifungulia mashtaka. Kwa muda wa miezi tisa, nilishirikiana na kila hatua ya uchunguzi wao, nilitoa taarifa zote”.
“Nakanusha mashtaka kwa ujumla wake na nitapambana kwa kila pumzi kusafisha jina langu. Kutokana na mchakato unaoendelea, sitatoa maoni yoyote zaidi”.