HABARI KUU
Aliyekuwa mgombea urais wa chama cha Republican Nikki Haley amesema ana mpango wa kumpigia kura Donald Trump, mpinzani wake wa zamani na bosi wake, katika uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka 2024.
Haley, ambaye aliwahi kuwa balozi wa Trump katika Umoja wa Mataifa, ambapo Haley alikuwa mpinzani wa mwisho kujiondoa katika kinyang’anyiro cha mchujo katika chama cha repablikani mapema mwezi machi.
Ambapo Siku ya Jumatano, katika matamshi yake ya kwanza hadharani tangu aondoke kwenye kinyang’anyiro hicho, alisema Trump “hajawa mkamilifu”, lakini Rais Joe Biden “amekuwa janga katika taifa la marekani”
Wapiga kura wa chama cha Republican wanaompinga Trump kwa kiasi kikubwa walikuwa nyuma ya azma ya Haley kuwania urais mapema mwaka huu, na bado anaungwa mkono zaidi ya miezi miwili hata baada ya kuondoka kwenye kinyang’anyiro hicho.
Ambapo Haley alishinda zaidi ya 20% ya kura katika takriban chaguzi mbili za awali za majimbo katika wiki mbili zilizopita.