UCHAMBUZI
Ukweli mwingine ambao sioni watu wakiusema ni kwamba kilichomuondoa Pochettino ni sawa na kilichomuondoa Thomas Tuchel, ni makubaliano ya pande zote mbili. Yani wamiliki wanasema tunataka timu tuiendeshe kwa mfumo huu, kocha anasema hapana tuiendeshe kwa mfumo huu. Pochettino hajafukuzwa, ni kushindwa kufikia makubaliano kwa pande zote mbili.
Lakini pia hii ndiyo maana na mantiki kubwa ya kuwa na watu wanaoitwa Sporting Director, wao ndiyo wanaisimamia timu kwa ukubwa, kazi ya kocha inabaki kuiongoza timu uwanjani tu.
Lakini falsafa na mipango yote inapandikizwa na hao ma-Sporting Director, wao ndiyo wamekuja na mfumo wa kutumia wachezaji wadogo kiumri na ndiyo wanaendeleza kusajili kama akina Estevao Willian.
Timu yako ikiwa na hawa ma-Sporting Director ni rahisi sana kocha kufukuzwa muda wowote sababu mipango yote imeshikiliwa na hao ma-Sporting Director, kazi ya kocha inakuwa kuletewa tu wachezaji na hata kama akihusika kwenye sajili basi hana sauti kama walivyo hawa ma-Sporting Director.
Na sio kama ni mfumo ulioanza leo pale Chelsea, ni mfumo uliokuwepo toka enzi za Roman Abramovich lakini pia unatumiwa na klabu nyingi duniani.