TB Joshua na sakata la kuwanyanyasa wanawake kingono

0:00

HABARI KUU

BBC World Service wamegundundua madudu ya nabii Joshua.

TB Joshua ahusishwa na skendo nzito ya unyanysaji, ubakaji, kuwapa mimba na kuwatoa mimba kinguvu wafuasi wake, vipigo na kutengeneza miujiza feki na shuhuda za uongo za uponyaji ili kuhadaa umma kwa miaka mingi

BBC Africa Eye ndio imeachia uchunguzi huo maalum, documentary ya zaidi ya dakika 150 yenye sehemu tatu, imesema imeufanya uchunguzi kwa miaka miwili kuhusu nabii huyo maarufu wa Nigeria wa kanisa la Synagogue Church Of All Nations

BBC Africa Eye imeweka wazi kuwa uchunguzi wao na interviews na wahanga mbalimbali ulianza mapema tu ila haukupita muda mrefu ndio Nabii huyo akafariki bila kutarajiwa 2021

BBC imefanya mahojiano na watu si chini ya 25 waliokuwa wafuasi wa karibu sana wa TB Joshua aliokuwa akiishi nao pamoja na wafanyakazi wa zamani wa kanisa hilo maarufu ambao wametoka nchi za Nigeria, Namibia, S.Africa, Ghana, Uingereza, Marekani na Ujerumani japokuwa TB Joshua alikuwa na wafuasi hao maalum wa karibu alioishi nao takribani 150

Wakihojiwa na waandishi 15 wa BBC kutoka nchi mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti katika uchunguzi huo wa muda mrefu, Wahanga wamesema kijuujuu watu wanaweza wasiwaamini ila wamedai kuwa TB Joshua hakuwa mtumishi wa kweli wa Mungu kama wengi walivyodhani machoni

Wahanga mbalimbali ambao ni wa kike wamesema walianza kufika kanisani hapo na kunyanyaswa kingono wakiwa bado hata hawajafikisha miaka 18, walibakwa na kutolewa mimba kinguvu zaidi ya mara moja na TB Joshua. wahanga wengine hawakutaka utambulisho wao kuwa wazi kwa sababu za kiusalama ila mhanga kwa jina la Jesca kutoka Namibia huku akilia amesema alianza kunyanyaswa akiwa na miaka 17 na hatimaye alitolewa mimba tano

Wengine wamesema walishajaribu kutaka kujiua walipokuwa katika himaya ya TB Joshua kwasababu ya ukatili waliopitia. Mmoja wa wahanga aliyetaka kukiua amesema kinachomuuma zaidi ni kuwa ashafariki bila sheria kuchukua mkondo wake

Paul aliyekuwa mmoja watu wa karibu sana wa TB Joshua amesema yeye alikuwa miongoni mwa manabii wa mwanzo wa kanisa hilo tangu 1995 hadi 2006 amedai TB Joshua moja ya mikakati yake mikubwa ilikuwa kuwavuta na kuwapata wafuasi wa kizungu kutoka mataifa ya nje ili kuzidi kuaminisha watu uponyaji wake kwani wengi wanaamini kuvuta mzungu karibu ni mafanikio ya kuvuta watu wengi zaidi waamini, amesema TB Joshua miaka hiyo alipata mgeni mchungaji wa S.Africa na wakati akiondoka alimpa mikanda ya VHS ya videos 200 wakaigawe nchi za kigeni ili watu waone miujiza

Na baadhi wahanga wa kigeni waliohojiwa na wao wakiwa bado vijana wengine miaka 17 wakati huo wamesema walianza kuona videos za maombi ya miujiza na shuhuda watu wakidai kupona magonjwa mbalimbali yakiwemo kansa, HIV na me ngineyo na ndio na wao wakaja, wahanga na baadhi ya wafanyakazi wa kanisa wamesema kimsimgi miujiza ya uponyaji iliyokuwa ikioneshwa kwa watu ni ya uongo wakieleza kwamba watu waliitwa kufunzwa kuigiza na kulipwa ili wahadae watu kuwa wamepona magonjwa hatari kama kansa, HIV

Wafuasi wa kigeni waliokuja Nigeria kwa wakati huo ambao ni sehemu ya wahanga wamesema pesa za nauli hawakutoa wao bali ziligharamiwa na TB Joshua na washirika wake wa makanisa mengine ya nje ikiwemo Uingereza ambao walisaidia kuwaleta hao wafuasi wa kizungu kwa TB joshua ambao wengi walikaa huko si chini ya miaka 10

Waliotolewa mimba mara kwa mara wamesema waliweza kuendelea kunusurika kwasababu nyuma ya pazia dawa zilitumika wakapewa kunywa wapone sio miujiza

Kwanini walishindwa kutoroka mapema?

wamesema ni kama walikuwa wamezubaishwa na kuvurugwa kisaikolojia wakawa sio wao, pia wamesmesa walikuwa wakipewa vitisho vikali na wengine kupigwa na kujeruhiwa watoto waliopelekwa na wazazi ili wapate mafunzo ya kiroho nao imeelezwa walipihwa na mikanda

Raia wa kigeni wamesema walitolewa bastola na walinzi wa maeneo ya kanisani kwa TB Joshua na wengine kutuma videos za ushahidi

Mwandishi wa habari BBC alijaribu kurekodi moja ya matukio alidakwa na kuwekwa kizuizini kwa masaa kadhaa na walinzi wa nabii huyo

Wahanga wamesema.hawakuwa wakiruhusiwa mawasiliano ya simu wala ya email ambayo yangekuwa rahisi kuwasiliana na ndugu na marafiki zao. Wahanga wa Uingereza wamesema walijaribu kuripoti kwa ofisi yao nchini humo lakini hakuna kilichofanyika

Aliyekuwa nabii katika synagogue hiyo amesema yeye tangu 2009 alitaka kupaza sauti kuileza jamii hali halisi kinachoendelea kwa mtu wanayemuona ni mtumishi wa Mungu lakini amesema alijaribu kuzibwa mdomo na kuaza kufuatiliwa na watu wa TB Joshua na wafuasi wake kindakindaki wakiwa wanadhani anataka kumchafua tu mtumishi wao kwa chuki binafsi, baada ya hapo amesema kwa miaka 8 akawa kwenye maisha ya kujifichaficha

Wahanga wengine wamekiri nguvu kutumika kuwanyamazisha kila walipotaka kuweka wazi kinachoendelea kwa muda mrefu

Wamesema TB joshua aliaminika kirahisi machoni pa wengi kwasababu ya kuisadia jamii misaada mbalimbi japo watu hawakujua kinachoendelea nyuma ya pazia

Uchunguzi huo pia umeangazia kwa undani kuporomoka kwa jengo la gorofa 6 mwaka 2014 lililotumika kulaza wafuasi wa nchi za kigeni hasa kutoka Ulaya na America ambalo mmiliki alikuwa TB Joshua..Watu 116 walitajwa kufariki kwa wakati huo lilipoporomoka ingawa wahanga waliohojiwa sasa wamesema idadi ni zaidi.ya waliotajwa uchunguzi huru ukifanywa tena, kwa wakati huo TB Joshu alidaiwa kutotoa ushirikiano wa kutosha kwa mamlaka za kiuchunguzi jengo lilipoporomoka na vyombo vingine vya habari vilihisi kuna kitu kinafichwa

Yaliyoelezwa ni mengi, kwenye uchunguzi, ila wengine wamemkingia kifua TB Joshua kuwa anasimgiziwa tu akiwemo Vimbai mtangazaji maarufu wa Zimbabwe aleyedai TB alikuwa mtu mzuri sana alimsaidia wakati wa msiba wa dada yake

TB Joshua aliyekuwa na wafuasi wengi nchi nyingi, hata hivyo enzi za uhai wake ilikuwa ikielezwa jumuiya za kikiristo nchini Nigeria ni kama zilikuwa zimejitenga nae muda mrefu hata kwenye mazishi yake

Baada ya uchunguzi wa BBC Africa Eye, mhadhiri wa kike kwa jina la Gloria toka chuo kikiuu kimojawapo Nigeria amesema kuna siku yeye aliwahi kulala katika viunga vya kanisa la TB Joshua lakini hata yeye alihisi kuna mambo ya kutilia shaka hayapo sawa hivyo haishangai sana taafifa ya kiuchunguzi ya BBC

Hata hivyo, wafuasi wa TB Joshua wanasema anasingiziwa na kuchaguliwa yanayosemwa hayana ukweli

Kanisa hilo kwasasa linaongozwa na mke wake, halijajibu madai ya ukatili na unyanyasaji yaliyoibuliwa na BBC Africa Eye kupitia mahojiano na wahanga ila kanisa limekana TB Joshua kuhusika na yaliyoelezwa kwa maelezo kuwa nabii huyo alishasemwa kwa mengi mabaya hata enzi za uhai wake.

See also  Dodgers and fans relish festive World Series parade

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

KITUKO CHA BODI YA LIGI DHIDI YA...
MICHEZO Siku moja tangu kamati ya kusimamia na kuendesha bodi...
Read more
Why Biologically Women are More Cleverly In...
LESSONS FOR YOUNG MEN. Women are born manipulators but men are...
Read more
SERIKALI YAWAITA WAWEKEZAJI KWENYE SGR
HABARI KUU Shirika la Reli Tanzania (TRC) limechukua hatua muhimu...
Read more
Pochettino akerwa na kichapo kutoka kwa Arsenal
MICHEZO Baada ya kichapo cha mabao 5-0 walichokipokea Chelsea kutoka...
Read more
Social media sensation Anwulika Udanoh and David...
In an unexpected twist, the union of Anwulika Udanoh and...
Read more

Leave a Reply