WANAFUNZI WAFARIKI KWA KUVUTA MOSHI WA JENERETA

0

0:00

HABARI KUU

Wanafunzi saba wa chuo kikuu wamefariki dunia baada ya kuvuta moshi wa jenereta katika studio ya muziki kwenye jimbo lenye utajiri wa mafuta la Bayelsa nchini Nigeria.

Vijana hao wanasemekana kufanya kazi hadi Jumatatu usiku na kulala kwenye studio iliyofungwa milango huku jenereta likiendelea kufanya kazi.

Wanashukiwa kufa kwa kukosa hewa safi na badala yake kuvuta hewa ya kaboni monoksaidi, lakini polisi wanasema uchunguzi unaendelea.

Sehemu nyingi za biashara na kaya nyingi nchini Nigeria zinategemea majenereta yanayotumia dizeli au petroli kutokana na nchi hiyo kukumbwa na mgawo wa umeme kwa kuwa unaozalishwa unatosheleza asilimia 60 tu ya mahitaji kwa sasa.

Miili sita iligunduliwa Jumanne asubuhi, huku mmoja wao alikuwa amepoteza fahamu, alikimbizwa katika hospitali ya karibu lakini alifariki dunia baadaye, vyombo vya habari viliripoti.

Wakazi wa eneo hilo walipiga kelele walipochungulia kupitia dirisha la studio hiyo na kuona miili ya vijana hao ikiwa sakafuni.

“Uchunguzi unaendelea lakini kulingana na kile tulichoona, sumu ya kaboni monoksaidi kutokana na moshi wa jenereta ni sababu inayoweza kuwa sababu ya vifo vyao” msemaji wa Jeshi la Polisi, Musa Mohammed ameambia BBC.

Vijana hao walikuwa ni wanafunzi wa shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Niger Delta (NDU) kinachomilikiwa na serikali huko Amassoma, ambao walikuwa pis wakijihusisha na biashara ya kurekodi muziki ili kupata pesa ya kuchangia gharama za masomo yao.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Peter Obi criticizes Tinubu's administration for proposing to spend N10 billion on constructing a car park and other facilities in the national assembly
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading