Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Patrice Motsepe amesema goli walilofunga Yanga SC dhidi ya Mamelodi Sundowns lililokataliwa lilikuwa halali.
Motsepe amesema hayo leo visiwani Zanzibar alipowasili kwa ajili ya kushuhudia michezo ya fainali ya mashindano michuano ya soka kwa shule za Afrika (African Schools Football) ambazo zitachezwa leo katika Uwanja wa New Amaan.
Amesema kuwa yeye kama Rais wa CAF hakupaswa kutoa maoni lakini “kama shabiki wa mpira, nilipotazama, lilikuwa ni goli.”
Kufuatia kukataliwa kwa goli hilo, timu hizo zilimaliza michezo yote miwili ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika bila kufungana, na Yanga ikatolewa kwa mikwaju ya penati baada ya kufungwa penati 3-2.
Katika fainali hizo, timu ya soka ya wavulana ya Tanzania itacheza dhidi ya Guinea, huku upande wa wasichana Morocco itakutana na Afrika Kusini.